
VITA YA KUZUIA KIFO | Mabadiliko ya tabianchi yanavyotishia kutoweka jamii za asili Tanzania
Miaka 30 iliyopita ilikuwa ni rahisi kwa jamii za Wahadzabe kupata maji karibu na maeneo walipokuwa wakiishi. Licha ya kuishi milimani, wakati huo kulikuwa na chemchemi na vijito vinavyotiririsha maji hadi nyakati za kiangazi.Iliwachukua muda mfupi tu kupata maji, matunda na wanyama pori kwa ajili ya chakula.Sasa hali imebadilika. Maeneo wanayoishi hususan katika bonde la Ziwa Eyasi yamekuwa yakikabiliwa na vipindi vya ukame na mvua zisizotabirika mara kwa mara na sehemu kubwa ya vyanzo vya maji vimekauka. Chemchem, vijito na baadhi ya mito ya karibu iliyokuwa ikitiririsha maji imekauka…
The skinny
The skinny isn't ready yet — notes appear once the transcript is processed.